SHERIA NA MAZINGIRA
Kitivo cha Sheria-RUCU kimechukua hatua ya kipekee katika kutenda haki na kulinda mazingira kwa kuanzisha mpango wa upandaji miti chuoni. Miti hii itabaki kama alama endelevu kwa vizazi vijavyo, ikionyesha dhamira ya kitivo katika kuunda mazingira rafiki na endelevu kwa wanafunzi.
Zoezi hili limeongozwa na uongozi wa Kitivo cha Sheria, likishirikisha wakufunzi na wanafunzi, wakiongozwa na viongozi wa Law Society. Mpango huu unalenga kuhimiza uwajibikaji wa kisheria, kuendeleza utunzaji wa mazingira, na kutoa nafasi kwa wanafunzi kujifunza na kuendeleza elimu yao ya kisheria katika mazingira salama na rafiki kwa mafunzo. Kitivo kinawaalika wanafunzi, wafanyakazi, na wadau kuendeleza jitihada za kutunza mazingira kwa kizazi kijacho.
Source: Faculty of Law