• PRO
  • 25 Jan 2026
  • RUCU-IRINGA

ZIARA YA KIMASOMO

Wanafunzi wa Sekondari ya St. James Kilolo wametembelea Chuo Kikuu Katoliki Ruaha (RUCU) na kujionea mazingira pamoja na miundombinu ya kisasa ya kufundishia na kujifunzia. Ziara imewapa picha ya karibu kuhusu namna elimu ya juu inavyowaandaa wataalamu wa siku zijazo.

Wanafunzi wameelimishwa kuhusu uhusiano kati ya masomo yao ya sekondari na safari ya kujenga “career path” yenye mwelekeo na malengo. Ziara imewapa mtazamo mpana kuhusu fursa za kitaaluma na umuhimu wa kufanya maamuzi sahihi mapema.

Wamehamasishwa kusoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zao za kuwa wataalamu katika fani za Afya, TEHAMA, Biashara, Uchumi, Elimu, Sheria na Uhandisi wa TEHAMA ambazo zinatolewa RUCU.

RUCU kinaendelea kukaribisha shule na wadau kutembelea,kujifunza, kubadilishana uzoefu, kuanzisha na kudumisha mahusiano.


Source: PRO's OFFICE

Advertisement